Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SENETA-SIASA

Maseneta nchini Marekani watofautiana kuhusu mashahidi dhidi ya Trump

Maseneta wa chama cha Democratic nchini Marekani, wamesema hawawezi kukubali kubadilishana mashahidi na chama cha Republican, katika mchakato wa kesi ya kumwondoa madarakani rais Donald Trump inayoendelea mbele ya Kamati ya Baraza la Senate.

Baraza la Senate nchini Marekani
Baraza la Senate nchini Marekani REUTERS/U.S. Senate TV/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mshauri ya rais Trump kuhusu masuala ya usalama John Bolton, ni miongoni mwa mashahidi ambao Maseneta wa chama Democratic wanasema atakuwa mtu muhimu sana katika kesi hii.

Hata hivyo, Maseneta hao wamekaa mtoto wa aliyekuwa Makamu wa rais Joe Biden kuwa shahidi.

Rais Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake lakini pia kudharau bunge na hivyo chama cha Democratic kinashinikiza kuondolewa kwake madarakani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwezi Novemba.

Trump, ameendelea kukanusha madai hayo na hata baada ya kurejea kutoka mjini Davos alikokuwa amehudhuria jukwaa la kiuchumi, hajazungumzia suala hili baada ya kurejea nyumbani.

Kumwondoa  madarakani katika baraza hilo lenye Masenta 100, inabidi Maseneta 67 wabunge mkono hoja hiyo.

Chama cha Democratic ambacho kinashinikiza kuondolewa madarakani kwa rais Trump kina Maseneta 47 kwa hivyo kinahitaji Maseneta 20 kutoka chama cha Republican ili kufanikiwa katika mchakato huu wa kihistoria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.