Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Baraza la Seneti la Marekani lafungua rasmi kesi ya ung'atuzi dhidi ya Trump

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya rais wa Marekani Donald Trump imeanza kusikilizwa rasmi mbele ya Baraza la la Seneti la Marekani tangu Alhamisi, Januari 16.

Maseneta wa Marekani wameapishwa kumhukumu rais Donald trump bila upendeleo, kulingana na Katiba, Alhamisi, Januari 16.
Maseneta wa Marekani wameapishwa kumhukumu rais Donald trump bila upendeleo, kulingana na Katiba, Alhamisi, Januari 16. REUTERS/U.S. Senate TV/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Maseneta watakaomhukumu rais Donald Trump waliapishwa wakati wa kikao maalum, baada ya mkuu wa Mahakama John Roberts kuingia kwenye makao makuu ya Baraza la Seneti kuanza kusikiliza kesi.

Hakimu mkuu katika taifa hilo mwenyewe alikuwa kiapo akishikilia bibilia kwa mkono wake wa kulia na wakati mwingine alionekana akisita alipokuwa akila kiapo.

Ikumbukwe kwamba hii ni mara ya tatu tu katika historia ya Marekani tukio kama hilo linatokea kwenye makao makuu ya Baraza la Seneti (Capitol).

Maseneta 100 wa Marekani, wote wamesimama, huku wakiinua mkono wa kulia na kula kiapo kwa kumhukumu rais wa Marekani bila upendeleo, kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.

Kabla ya kesi hiyo kuanza, Wabunge 7 wa chama cha Democratic walioteuliwa walioteuliwa kwa kuendesha mashtaka ya kesi dhidi ya Trump walisoma mashitaka yanayomkabili mshtumiwa.

Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi.

Kesi hiyo imepangiwa kuanza kusikilizwa Januari 21.

Donald Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia bunge.

Democrats wanadai kwamba Rais alizuia Dola milioni 391 za msaada wa kijeshi ili kushinikiza Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden.

Hata hivyo amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni madai ya udanganyifu.

Trump ni rais wa tatu kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye. Marais wawili wa kwanza ni Andrew Johnson na Bill Clinton ambao hawakuondolewa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.