Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Wabunge wateuliwa kwa kuendesha mashtaka ya kesi dhidi ya Trump

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha azimio la kuwasilisha mashtaka dhidi ya rais Donald Trump katika Bunge la Seneti. Hatua hii inaashiria kuanza kwa kesi inayoweza kumuondoa madarakani rais huyo.

Wabunge saba kutoka chama cha Democratic walioteuliwa kuendesha mashtaka katika kesi ya Trump mbele ya Bunge la Seneti. Wataongozwa na Adam Schiff, mwendesha mashtaka mkuu katika mashtaka ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump.
Wabunge saba kutoka chama cha Democratic walioteuliwa kuendesha mashtaka katika kesi ya Trump mbele ya Bunge la Seneti. Wataongozwa na Adam Schiff, mwendesha mashtaka mkuu katika mashtaka ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump. OLIVIER DOULIERY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wabunge 228 walipitisha azimio hilo huku 193 wakipinga.

Hii inamanaisha kuwa, bunge la Senate ambalo linadhibitiwa na Maseneta wa chama cha rais Trump cha Republican watapata nafasi ya kusikiliza madai ya Trump na kuyapigia kura.

Hatua hiyo imekuja katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, tangu wabunge wa baraza hilo kumkuta na hatia Rais Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia juhudi za Bunge kuchunguza vitendo vyake.

Mwaka ulipita, Bunge la Wawakilishi ambalo linaongozwa na chama cha Democratic, walipigia kura ya kumwondoa madarakani rais Trump kwa kutumia vibaya madaraka yake lakini pia, kudharau bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.