Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Bunge la Seneti kupokea mashtaka ya Trump, kesi kuanza

media Spika wa Baraza la Wawakilishi na mpinzani mkuu wa Donald Trump, Nancy Pelosi, alitangaza Jumanne wiki hii baada ya mkutano faragha na wabunge kwamba mashtaka yanayomkabili Donald Trump yatapelekwa mbele ya Bunge la Seneti Jumatano Januari 15. REUTERS/Erin Scott

Baada ya wiki kadhaa, hatimaye Baraza la Wawakilishi linataraji kupiga kura leo Jumatano kupeleka mashtaka dhidi ya Donald Trump mbele ya Bunge la Seneti.

Hii ni hatua ya mwisho kabla ya kuanza kwa kesi ya ung'atuzi dhidi ya rais huyo kutoka chama cha Republican.

Spika wa Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Democratic na mpinzani mkuu wa Donald Trump katika baraza hilo, Nancy Pelosi, alitangaza Jumanne wiki hii baada ya mkutano faragha na wabunge kwamba mashtaka yanayomkabili Donald Trump yatapelekwa mbele ya Bunge la Seneti leo Jumatano Januari 15.

Bunge la seneti linadhibitiwa na chama cha Republican cha Donald Trump. Wadadisi wanasema ni vigumu bunge hilo lipitishe mashitaka hayo ya rais kutoka chama kinachodhibiti taasisi hiyo kubwa nchini Marekani.

Donald Trump anakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia Bunge kufanya shughuli zake.

Upinzani unaamini kwamba rais Donald Trump alitumia rasilimali za serikali kushinikiza Ukraine kuchunguza mgombea urais kutoka chama cha Democratic Joe Biden, mpinzani wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba. Upinzani unamshtumu haswa kwamba alizuia msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo iliyo katika mgogoro wa kijeshi na jirani yake Urusi, ili kufanikisha malengo yake.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana