Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Baraza la Congress kuanza kuandaa mashtaka dhidi ya Trump

Spika wa Baraza la Congress nchini Marekani Nancy Pelosi, kutoka chama cha Democratic, amesema baraza hilo litawasilisha mashtaka ya uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump, kwa madai ya 'matumizi mabaya ya mamlaka yake'.

Nancy Pelosi, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, anataka kuandaliwa mashtaka dhidi ya Donald Trump, Alhamisi Desemba 5, 2019.
Nancy Pelosi, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, anataka kuandaliwa mashtaka dhidi ya Donald Trump, Alhamisi Desemba 5, 2019. REUTERS/Erin Scott
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amepuuzia mbali kauli hiyo na kubaini kwamba analengwa kisiasa.

"Tutashinda" vita, amesema Donald Trump, huku akibaini kwamba ana imani na Bunge la Seneti kuwa halitamuangusha.

Bunge la Seneti linatawaliwa na idadi kubwa ya wajumbe kutoka chama cha Republican.

Trump amesema kuwa ana imani kuwa bunge hilo litafutilia mbali madai hayo.

Katika hotuba yake, Nancy Pelosi ameomba kamati ya masuala ya sheria ya bunge, inayodhibitiwa na chama cha Democratic kuanza kuandaa mashtaka.

"Rais hana tena nafasi kwa sababu alijaribu tena kuchafua uchaguzi wetu kwa maslahi yake binafsi," Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema.

"Alitumia vibaya madaraka yake, akadhoofisha usalama wa taifa letu na alihatarisha uhuru wa uchaguzi wetu," Bi Pelozi ameongeza.

Hatua hii imekuja, baada ya kumaliza kwa uchunguzi ambao kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na bunge, rais Trump aliwasiliana na kiongozi wa Ukraine kwa ajili ya maslahi yake ya kisiasa ili kupata usaidizi wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.Hatua hii imekuja, baada ya kumaliza kwa uchunguzi ambao kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na bunge, rais Trump aliwasiliana na kiongozi wa Ukraine kwa ajili ya maslahi yake ya kisiasa ili kupata usaidizi wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Hatua hii imekuja, baada ya kumaliza kwa uchunguzi ambao kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na bunge, rais Trump aliwasiliana na kiongozi wa Ukraine kwa ajili ya maslahi yake ya kisiasa ili kupata usaidizi wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Kauli ya bi Pelosi inakuja siku moja baada ya kamati ya masuala ya sheria ya bunge kuanza kuangalia mashitaka yanayoweza kuwasilishwa dhidi ya rais huyo kutoka chama cha Republican.

Hata hivyo Donald Trump aliwaambia Wademokrats kama watataka kumshitaki basi waharakishe.

Hata hivyo, rais Trump ameendelea kukanusha madai yake dhidi yake na kusema yanatumiwa kisiasa na wapinzani wake kutoka chama chsa Democratic.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.