Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya Trump: Baraza la Wawakilishi kuanza mjadala wa kisheria

Baada ya uchunguzi wa miezi miwili, Baraza la Wawakilishi nchini Marekani linaanza leo Jumatano mjadala wa kisheria kwa kuzingatia 'ushahidi wa kutosha' ambao wabunge kutoka chama cha Democratic wanasema wamekusanyika dhidi ya rais wa Marekani.

Donald Trump aendelea kukabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya kwa minajili ya kuchaguliwa kwake tena.
Donald Trump aendelea kukabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya kwa minajili ya kuchaguliwa kwake tena. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Wengi wanajiulizi iwapo tuhuma dhidi ya Trump zina ushahidi wa kutosha kuhalalisha kutimuliwa kwake madarakani.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye ametangaza kwamba mchakato unaomlenga unaendeshwa kisiasa, amesema hakufanya chochote kibaya katika kuomba Ukraine imchunguze Joe Biden, mmoja wa wapinzani wake wakuu katika uchaguzi wa urais wa mwama 2020.

Lakini chama cha upinzani cha Democratic kinaamini kwamba Donald Trump alitumia vibaya madaraka yake kwa kutaka aweze kuchaguliwa tena kama rais, kwa kuzuia msaada wa kijeshi wa karibu dola milioni 400 kwa nchi ya Ukraine ambayo ina mzozo na Urusi.

Baraza la Wawakilishi ambalo linatawaliwa na idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha Democratic, lilizindua mchakato wa ung'atuzi dhidi ya Donald Trump mwishoni mwa mwezi Septemba, na Kamati ya upelelezi katika Bunge kupewa jukumu la kuchunguza madai hayo.

Baada ya kuwahoji mashuhuda kumi na tano, kamati hiyo ilihitimisha katika ripoti ya uchunguzi iliyochapishwa Jumanne kwamba Donald Trump "aliweka mbele masilahi yake binafsi na kisiasa badala ya masilahi ya taifa, huku akitaka kudhoofisha uhuru wa mchakato wa uchaguzi na kutaka kuhatarisha usalama wa taifa ".

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna "ushahidi wa kutosha" wa tabia "isiyofaa" katika mambo yote mawili: "rais Trump amekuwa akitafuta msaada kutoka nje ya nchi hasa nchini Ukraine, kumsaidia kuchaguliwa tena wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 "na" alizuia "uchunguzi wa bunge."

“Ni hatari sana kwa nchi kuwa na rais asiye na maadili, ambaye anaamini yuko juu ya sheria," amesema mbunge kutoka chama cha Democratic, Adam Schiff, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya upelelezi katika Baraza la Congress.

Hata hivyo, rais Trump ameendelea kukanusha madai hayo na kusema, ni vita vya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.