Pata taarifa kuu
BRAZILI-LULA-HAKI

Brazil: Rais wa zamani wa Brazil kuachiliwa huru

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, ambaye anazuiliwa jela kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa makosa ya rushwa, hivi karibuni anaweza kuachiliwa huru baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu Alhamisi usiku.

Majaji wa Mahakama Kuu ya Brazil wakijadili uamuzi wa kuchukua kuhusu kesi ya rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva, tarehe 4 Aprili, 2018 Brasilia.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Brazil wakijadili uamuzi wa kuchukua kuhusu kesi ya rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva, tarehe 4 Aprili, 2018 Brasilia. AFP
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Brazil wamepiga kura ya kubadilisha kanuni ambayo imekuwa ikitaka wafungwa ambao hupoteza rufaa ya kwanza, kufungwa jela.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa, hatua hii huenda ikasababisha rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva kuwa huru.

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakati wa mahojiano yake ya kwanza tangu kufungwa kwake katika makao makuu ya Polisi, Curitiba,  Aprili 26, 2019.
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakati wa mahojiano yake ya kwanza tangu kufungwa kwake katika makao makuu ya Polisi, Curitiba, Aprili 26, 2019. Isabella LANAVE / El Pais / AFP

Aidha, uamuuzi huu unamaanisha kuwa, maelfu ya wafungwa wakaachiliwa huru.

Uamuzi wa majaji 11 wa Mahakama Kuu ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na gamu na tayari umetolewa, baada ya mjadala mrefu, kwa kura 6 dhidi ya 5, na unaweza kuwaachilia huru wafungwa wengine 5,000.

Lula, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 8 na na miezi 10 jela kwa makosa ya ufisadi, alifungwa jela mwezi Aprili 2018, muda mfupi baada ya hukumu dhidi yake kuthibitishwa na Mahakama ya Rufaa, ingawa bado anaendelea kukataa rufaa katika mahakama za juu.

Mara tu baada ya uamuzi huo kutolewa, mawakili wa kiongozi huyo wa kihistoriakutoka mrengo wa kushoto nchini Brazil wametangaza kwamba wanataka kuomba mteja wao aweze kuachiliwa huru.

Lula anazuliwa jela kwa siku 579.

Waendesha mashtaka wanaohusika na uchunguzi huo wamesema kwa taarifa kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu unaenda kinyume na "hisia za kutokujali kuadhibu" na umuhimu "wa mapambano dhidi ya ufisadi, ambavyo ni vipaumbele kwa nchi yetu ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.