Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Joe Biden aongelea kuhusu ung'atuzi unaomlenga Donald Trump

media Joe Biden ni mmoja wa wapinzani wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020. REUTERS/Scott Morgan

Makamu wa rais wa zamani na mgombea urais nchini Marekani ametangaza kwa mara ya kwanza kwamba anaunga mkono utaratibu ulioanzishwa na washirika wake kutoka chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi.

Joe Biden ni chanzo cha kesi ambayo ilipelekea kuzinduliwa kwa uchunguzi kuhusu ung'atuzi unaomlenga Rais Donald Trump. Rais wa Marekani alijaribu kupata habari za kutatanisha zenye lengo la kumtia matatani Joe Biden kutoka kwa mwenzake wa Ukraine. Makamu wa rais wa zamani anakabiliwa na tuhuma za kila mara kutoka kwa Donald Trump, ambaye amemhusisha na uvumi usio na msingi na kumtuhumu kwa madai ya ufisadi. Lakini Joe Biden mpaka sasa alikuwa amekataa kuzungumzia chochote kuhusu kung'atuliwa madarakani kwa Donald Trump. Hatimaye amebadilisha msimamo baada ya ikulu ya White House kutangaza kukataa kushirikiana na Bunge.

"Rais Trump amejishtumu mwenyewe. Kwa kuzuia mahakama kufanya kazi, kwa kukataa kutii hoja za Baraza la Wawakilishi, tayari amejihukumu mwenyewe. Mbele ya ulimwengu na raia wa Marekani, Donald Trump amekiuka kiapo chake, amesaliti taifa lake. Ili kulinda Katiba yetu, demokrasia yetu, kanuni zetu za msingi, anapaswa kufanyiwa uchunguzi ili aweze kung'atuliwa madarakani, "

Donald Trump amejibu mara moja kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu hoja za mpinzani wake: alimwita Joe Biden kuwa mtu asiyefaa, na kuanzisha mashtaka mapya bila ushahidi.

Barua kutoka Ikulu ya White House kwa wabunge hao, ambao wengi ni kutoka chama cha Democratic, imesema uchunguzi huo hauna maana na ni kinyume cha katiba.

Trump amekuwa akisema kinachoendelea ni kumlenga na kumchafulia jina kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana