Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAMZA-USALAMA

Marekani: Hamza, mwana wa kiume wa Osama Bin Laden, amefariki dunia

Hamza bin Laden, mmoja wa wana wa Osama Bin Laden, ambaye alielezwa kuwa mrithi kwenye uongozi wa al-Qaida, amefariki dunia, na Marekani imechangia operesheni hiyo ya kumuangamiza, kulingana na makala yaliyochapishwa Jumatano na gazeti la Marekani la New York Times na NBC.

Hamza bin Laden, mtoto wa Osama bin Laden, amefariki dunia , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani.
Hamza bin Laden, mtoto wa Osama bin Laden, amefariki dunia , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani. FEDERATION FOR DEFENSE OF DEMOCRACIES / AFP
Matangazo ya kibiashara

NBC, moja ya vyombo vya habari vya kwanza vilivyothibitisha kifo hicho, imebaini kwamba Washington inana taarifa kutoka idara za ujasusi zinazothibitisha kifo cha Hamza Bin Laden, ikinukuu maafisa watatu ambao hawakutajwa majina.

"Sitaki kueleza chochote kuhusu taarifa hiyo," Rais Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari Jumatano, alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu taarifa hiyo ya NBC.

Kwa upande wake, gazeti la New York Times limedai kwamba Marekani "ilihusika" katika operesheni hiyo ya kuuawa kwa Hamza bin Laden, ambaye alichukuliwa kama kiongozi mkuu wa al-Qaida. Gazeti hilo limenukuu maafisa wawili wa Marekani.

NBC na New Yok Times hawakutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe, mahali au mazingira ya kifo chake. Kulingana na taarifa ya New York Times, tukio hilo lilitokea miaka miwili iliyopita, lakini Marekani ilisubiri muda mrefu ili iweze kuthibitisha.

Mnamo mwezi Februari mwaka huu Marekani ilitoa zawadi ya hadi dola milioni mmoja kwa mtu yeyote atakaye toa taarifa ya kupatikana kwa Hamza bin Laden. Mnamo mwezi Machi alinyang'anywa uraia wake wa Saudi Arabia.

Hamza Bin Laden, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa ujumbe mbalimbali wa sauti na video akitoa wito wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani na nchi nyingine.

Kadhalika alikuwa amewatolea wito watu wa rasi ya Arabia kulipiza kisasi. Saudi Arabia ilimyang'anya uraia mwezi Machi.

Aliaminika kuwa katika kifungo cha nyumbani nchini Iran lakini ripoti nyingine zilisema kuwa huenda alikuwa akiishi katika mataifa ya Afghanistan, Pakistan na Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.