Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Adhabu ya kunyogwa kurudi kutekelezwa Marekani

media Barr amesema wafungwa watano wanaotarajiwa kunyongwa walihukumiwa kwa makosa ya mauaji, ubakaji wa watoto na wazee. Brendan Smialowski / AFP

Serikali ya Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003 inatarajia kutekeleza adhabu ya kunyonga baada ya kuwa imesitisha kwa muda wa karibu miaka 16, imesema taarifa ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Katika taarifa yake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, William Barr, amesema ameiagiza idara ya magereza kupanga ratiba ya kunyongwa kwa wafungwa watano.

Barr amesema wafungwa hao walihukumiwa kwa makosa ya mauaji, ubakaji wa watoto na wazee.

Taarifa yake imesema baada ya majadiliano na mamlaka husika, wamekubaliana kuwa adhabu ya juu kwa wafungwa hao ni kunyongwa na kwamba Serikali itaendelea kuheshimu sheria za nchi kwa ajili ya kutenda haki kwa waathirika wa vitendo na wanafamilia.

Tayari mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamekashifu uamuzi huo wa Serikali ya Marekani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana