Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 22/11 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 22/11 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Donald Trump ataka kesi ya ung'atuzi dhidi yake kuanzishwa katika Bunge la Seneti (White House)
 • Bolivia: Serikali ya mpito yapinga dhidi harakati za Morales nchini Mexico
Amerika

Madawa ya kulevya: El Chapo ahukumiwa kifungo cha maisha jela Marekani

media Mlanguzi sugu wa madawa ya kulevya "El Chapo", Mexico Januari 2016. REUTERS/Tomas Bravo/File Photo

Mahakama ya serikali kuu mjini Brooklyn nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha maisha jela Joaquin "El Chapo" Guzman, mlanguzi sugu wa dawa za kulevya raia wa Mexico, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya kihalifu iliyosababisha vifo vya watu wengi na kuingiza nchini Marekani tani nyingi za madawa ya kulevya.

Guzman mwenye umri wa miaka 62, pia ameamriwa kulipa dola milioni 12.6. Guzman alipatikana na hatia Februari mwaka huu kwa kusafirisha Marekani tani za cocaine, heroin na bangi na kuhusika katika njama za mauaji wakati akiwa kiongozi wa mtandao maarufu nchini Mexico wa biashara ya madawa za kulevya wa Sinaloa.

Jaji wa Marekani Brian Cogan ametangaza hukumu hiyo ya maisha pamoja na miaka 30.

Mahakama ya Shirikisho New York imemkuta El Chapo na hatia katika makosa 10, ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya, utakatishaji fedha.

El Chapo alitoroko gerezani nchini Mexico mwaka 2016 na baadae kukamatwa na kuhamishiwa Marekani.

Mwezi Aprili 2017, baba mkwe wa Joaquin Guzman, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kupenyeza bangi nchini Marekani.

Ines Coronel Barreras alipatikana na makosa katika mahakama moja ya Mexico, baada ya polisi kutwaa magari silaha na zaidi ya kilo 250 za bangi.

Marekani ilimwekea vikwazo miaka sita iliyopita, na kusema kwamba ni mojawepo wa vigogo wa genge la Sinaloa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana