Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-USALAMA

Magari makubwa ya kijeshi kushirikishwa katika maadhimisho ya uhuru Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kubadili taswira ya maadhimisho ya uhuru wa nchi hiyo inayoadhimishwa tarehe 4 Julai kila mwaka. Hali ambayo imezua sintofahamu nchini humo.

Gari la kijeshi la Bradley limeegeshwa Julai 3, 2019 katika eneo la Lincoln Memorial kwa kusubiri maadhimisho ya Siku ya uhuru wa Marekani Julai 4, kama alivyoagiza rais Donald Trump.
Gari la kijeshi la Bradley limeegeshwa Julai 3, 2019 katika eneo la Lincoln Memorial kwa kusubiri maadhimisho ya Siku ya uhuru wa Marekani Julai 4, kama alivyoagiza rais Donald Trump. REUTERS/Jim Bourg
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump ameagiza magari makubwa ya kijeshi pamoja na ndege kushiriki katika gwaride la kijehi litakaloshuhudiwa na maelfu ya raia nchini Marekani.

Donald Trump anataka jeshi litumie vifaa vyake katika gwaride la siku ya kuadhimisha uhuru wa Marekani, siku ambayo inaadhimishwa Julai 4 kila mwaka.

Kwa mara ya kwanza magari makuu ya kivita yametakiwa kushiriki gwaride hilo.

Muda wa zoezi la kurusha itifaki utaongezwa baada ya ndege za kivita kualikwa kushiriki katika zoezi la Julai 4. "Nitasema maneno machache, siku hiyo tutashuhudia kwa macho yetu ndege za kivita zikipaa angani na kupita juu yetu," rais wa Marekani alisem amwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa upande wa chama cha Democratic chenye viti vingi bungeni, wanasema kwamba, hatua hiyo ya Donald Trump ni njia ya kuweka tukio hilo kwa manufaa yake, ikiwa imesalia karibu mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa urais wa 2020. Wabunge kutoka chama hicho wanataka pia kujua gharama ya tukio hili. Utawala wa Trump haujatoa jibu kwa swali hilo.

Viongozi wa Wilaya ya Columbia ambako kumepangwa kufanyika sherehe hizo wamesema mji wao haukukujengwa kwa kupokea vifaa kama hivyo, huku wakibaini kwamba magari makuu ya kivita ya kijeshi yataharibu barabara muhimu. "Magari hayo yatawekwa katika maeneo maalumu, amesema rais donald trump.

Hatua hii ya Donald Trump inakuja baada ya kuhudhuria gwaride la jeshi la Ufaransa wakati wa maadhimisho ya uhuru Julai 14, 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.