Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Donald Trump atetea uamuzi wake wa kuongeza ushuru kwa bidhaa kutoka China

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea uamuzi wa serikali kuongeza ushuru unaotozwa kwa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka nchini China, licha ya mshauri wake wa masuala ya kiuchumi kuonya kuwa hatua hii itasababisha pande zote kupata hasara.

Rais wa Marekani Donald Trumpaona kwamba hatua ya kuongeza ushuru kwenye bidhaa kutoka China itapelekea nchi yake kunufaika zaidi.
Rais wa Marekani Donald Trumpaona kwamba hatua ya kuongeza ushuru kwenye bidhaa kutoka China itapelekea nchi yake kunufaika zaidi. AFP PHOTO/Jim Watson
Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, rais Trump amesema hatua hiyo aliyoichukua wiki iliyopita, kuongeza ushuru kwa asilimia 25 ni sahihi kwa kile anachosema "hapo ndipo China inastahili kuwa".

Hata hivyo mshauri wake wa masuala ya uchumi Larry Kudlow, akihojiwa na Televisheni ya Fox News amesema pande zote zitaumizwa na hatua hii, na watakaoumizwa zaidi ni wafanyibiashara wala sio serikali ya China.

China huingiza bidhaa nchini Marekani zenye thamani ya Dola Bilioni 200 kila mwaka, na uongozi wa Trump umekuwa ukiona kuwa hakuna usawa wa kibiasahra kati ya nchi hizo mbili na hivyo kujaribu kufikia usawa huo, nyongeza ya ushuru imetoka asilimia 10 hadi 25.

Hadi sasa, China haijsema iwapo italipiza kisasi kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani na kuongeza mvutano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.