Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MADURO-SIASA-HAKI

Wabunge kadhaa wakamatwa Venezuela

Mahakama Kuu ya Haki imechukua uamuzi wa kuwavua kinga wabunge kadhaa wa upinzani kwa kuhusika kwao katika mapinduzi yaliyoshindikana wiki iliyopita.

Maikel Moreno, jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya Haki Venezuela, Mei 8, 2019.
Maikel Moreno, jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya Haki Venezuela, Mei 8, 2019. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa Luis Florido, ambaye ni miongoni mwa wabunge waliovuliwa kinga ya ubunge, amesema uamuzi huo unaonyesha ukiritimba wa utawala. "Aina hii ya uamuzi haitushangazi. Kwanza, inalenga kudhoofisha na kuhatarisha usalama wa taasisi pekee halali nchini Venezuela inayowakilisha Bunge la taifa lililochaguliwa mnamo mwaka 2015.

Uamuzi huu kwa kweli una lengo maalum ambalo ni kuzuia shughuli za Bunge ambalo linataka kuweka sawa na kuheshimisha Katiba.

Serikali ya Venezuela imesema itawafungulia mashtaka wabunge 10 waliounga mkono mapinduzi yaliyoshindikana juma lililopita. Mapinduzi ambayo yaliitishwa na kinara wa upinzani Juan Guaido.

Uamuzi wa Serikali ya Venezuela umekuja wakati huu ambapo Marekani imetangaza kuondoa vikwazo kwa viongozi wa kijeshi na mawaziri wa zamani walioachana na serikali ya rais Nicolas Maduro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.