Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Venezuela: Guaido aombwa kuvuliwa kinga ya ubunge

Mahakama Kuu ya Venezuela, ambayo iko chini ya udhibiti wa serikali ya rais wa Nicolas Maduro, imeomba kiongozi wa upinzani Juan Guaido, avuliwe kinga ya ubunge, ili aweze kufunguliwa mashitaka.

Spika wa Bunge la Venezuela na kiongozi wa upinzani, Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela..
Spika wa Bunge la Venezuela na kiongozi wa upinzani, Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela.. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Katika uamuzi uliotolewa Jumatatu wiki hii, mahakama ya juu nchini Venezuela imeomba Spika wa Bunge la Taifa lililowekwa na Maduro "kumvua kinga ya ubunge" Bw Guaido, anayetambuliwa kama rais wa mpito na nchi zaidi ya hamsini.

Mahakama Kuu na Bunge la taifa lililowekwa na MAduro linashtumiwa na upinzani kwamba ni vibaraka vya utawala uliopo madarakani.

Juan Guaido, ambaye ndiye Spika wa Bunge la Venezuela linalodhibitiwa na upinzani, anashutumiwa kukiuka marufuku aliyowekewa ya kuondoka nchini.

Mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 35 alifutilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu wa Januari 29, akiondoka nchini kinyume cha sheria na kufanya ziara katika nchi jirani za Colombia, Brazili, Paraguay, Argentina na Ecuador, mwishoni mwa mwezi Februari hadi mwanzoni mwa mwezi Machi.

Uamuzi huu unakuja wakati Nicolas Maduro na mpinzani wake mkuu wanaendelea kupigania madaraka tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika nchi ambayo inakumbwa na kiza kinene kufuatia kukatwa kwa umeme.

Hayo yanajiri wakati rais Maduro alimfuta kazi waziri wa nishati Jenerali muustafu Luis Motta Dominguez na nafasi yake imechukuliwa na Igor Gavidia Leon.

Luis Motta Dominguez amekua akihudumu kwenye nafasi hiyo tangu mwezi Agosti 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.