Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Boeing 737 MAX ya shirika la ndege la Southwest Airlines yatua kwa dharura

media Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la Southwest Airlines imelazimika kuttua kwa dharura kwenye uwanja wa kimataifa wa Orlando, California, kutokana na tatizo la kimitambo. REUTERS/Mike Blake

Ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la Southwest, iliyokuwa ikisafiri kwenda California kuegeshwa kutokana na marufuku yanayozikabili ndege hizo na ambayo haikuwa na abiria, imelazimika kutua kwa dharura, shirika hilo limesema.

Katika taarifa yake, Southwest Airlines imesema kuwa ndege hiyo ilijulikana kuwa ina tatizo la kimitambo lisilo husiana na lile linalochunguzwa kama sababu ya ajali ya ndege mbili za aina hiyo ya Boeing 737 MAX, nchini Ethiopia mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi na indonesia mwezi Oktoba mwaka jana.

"Wafanyakazi wa ndege hiyo walifuatilia maelekezo na kulazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orlando na wote wako salama. Ndege hiyo ililazimika kutua baada ya kuona kuwa inatatizo kwenye moja ya injini zake, shirikala ndege la Southwest Airlines limebaini.

Ndege hiyo ilitarajiwa kusafiri kwenda uwanja wa ndege wa Victorville, huko California, karibu na jangwa la Mojave, eneo ambako Southwest ilianza kutuma ndege zake aina ya MAX kwa minajili ya kuhufadhiwa.

Kampuni ya Boeing imealika marubani zaidi ya 200, viongozi na wasimamizi mbalimbali kuhudhuria kikao cha mafunzo kuhusu mpango wake wa unaolenga kuunga mkono uanzilishwaji upya wa safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX, ambapo kampuni hiyo ya Marekani itatoa maelezo kuhusu kupitia upya programu ya Boeing 737 MAX.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana