Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Guaido aapa kurejea Venezuela Jumatatu hii

Kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa mpito nchini Venezuela na kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi Juan Guaidó, ameitisha maandamano ya wananchi wakati huu anaporejea nchini humo.

Juan Guaido akizungukwa na rais wa Colombia Ivan Duque (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Amerika, Luis Almagro (kushoto), wakitoa taarifa tya pamoja kwenye vyombo vya habari,  Cucuta, Jumamosi, Februari 23, 2019.
Juan Guaido akizungukwa na rais wa Colombia Ivan Duque (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Amerika, Luis Almagro (kushoto), wakitoa taarifa tya pamoja kwenye vyombo vya habari, Cucuta, Jumamosi, Februari 23, 2019. REUTERS/Luisa Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa upinzani alivuka mpaka mwezi uliopita na kuanza zira katika mataifa jirani na kukutana na Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence nchini Colombia lakini pia rais mpya wa Brazil Jair Bolsonaro.

Guaido ambaye sasa anatambuliwa na zaidi ya mataifa 50, ameendelea kushikiza kujiuzulu kwa rais Nicolas Maduro, na ametoa wito kwa maelfu ya raia wa nchi yake kujitokeza kwa wingi kuandamana leo Jumatatu.

Mwanasiasa huyo alifanikiwa kundoka nchini humo licha ya Mahakama ya Juu, kumzuia na sasa haijafamika atarudi vipi nchini Venezuela.

Mkuu wa sera ya Mambo ya Nje katika Umoja wa Ulaya Federica Mogherini ameonya kuwa, kumdhuru Guaido kutasabisha mvutano wa kisiasa kuwa mbaya zaidi.

Licha ya shinikizo hizi, rais Nicolas Maduro amesema hawezi kujiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.