Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Guaido aahidi kurudi Venezuela Jumatatu

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido, baada ya kukutana na rais wa Brazil Jair Bolsonaro jijini Brasilia amesema kuwa anapanga kurudi nchini Venezuela Jumatatu wiki ijayo licha ya "vitisho".

Kiongozi wa upinzani Venezuela, Juan Guaido.
Kiongozi wa upinzani Venezuela, Juan Guaido. REUTERS/Manaure Quintero
Matangazo ya kibiashara

Juan Guaido ambaye nchi zaidi ya hamsini zinamtambua kama rais wa mpito wa Venezuela aliondoka nchini Venezuela Februari 22 licha ya kupigwa marufuku kuondoka nchi humo, kwa hatari ya kukamatwa atakaporejea, kama alivyoonya rais Nicolas Maduro.

"Nimepata vitisho upande wangu na familia yangu, lakini pia nimepata vitisho vya kufungwa na serikali lakini hilo halinizuii kurudi Venezuela kabla ya Jumatatu," amesema kiongozi wa upinzani katika mkutano na waandishi wa habari.

Juan Guaido anatarajia kuondoka Brasilia mapema leo Ijumaa kwenda Paraguay.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.