Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-SIASA

Marekani: Makubaliano yafikiwa kuhusu bajeti, kuelekea kufadhili ujenzi wa ukuta

Marekani inapanga kuepuka kukwama tena kwa shughuli za serikali. Bunge la Wawakilishi limepitisha muswada wa fedha ambao tayari umeidhinishwa na Bunge la Seneti.

Kwenye mpaka wa Marekani na Mexiko, katika eneo la El Paso / Ciudad Juarez, ujenzi ukiendelea, Februari 5, 2019.
Kwenye mpaka wa Marekani na Mexiko, katika eneo la El Paso / Ciudad Juarez, ujenzi ukiendelea, Februari 5, 2019. REUTERS/Jose Luis Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House inatarajia kutia saini kwenye sheria ya bajeti hata kama nakala hiyo haizungumzii dola Bilioni 5.7 ambayo rais anahitaji kwa ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na Mexico.

Ili kupata fedha anazohitaji, rais Donald Trump anatarajia kutangaza hali ya dharura kwenye mpaka wa Marekani na Mexico. Hatua ambayo itamuwezesha kutopingwa na Bunge la Wawakilishi.

Muswada wa kifedha ulipitishwa Alhamisi wiki hii na idadi kubwa ya wajumbe wengi katika bunge la Seneti, linalodhibitiwa na chama cha Republican, na Bunge la Wawakilishi, lililoongozwa idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha Democratic, baada ya mjadala mkali. Muswada huo ulipitishwa na wabunge 300 dhidi ya 128 walioupinga.

"Rais atasaini muswada wa kifedha, lakini wakati huo huo atatangaza la hali ya dharura na nikamwambia kuwa nitaunga mkono hatua hiyo ya dharura, "amesema Seneta Mitch Mc Connell.

Hata hivyo awali wabunge wengi na maseneta kutoka chama cha Republican walitangaza kwamba watapinga tangoze lolote la Trump kuhusu hali ya dharura kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, kwa mujibu wa mwandishi wetu Washington, Anne Corpet.

Kwa upande wa kiongozi mkuu wa wabunge wa chama cha Democratic Nancy Pelosi, amesema ni matumizi tu mabaya ya madaraka kwa Rais Trump. "Kwanza, hakuna hali ya dharura kwenye mpaka, kuna changamoto ya kibinadamu tunayokabiliana nayo. Lakini mbali na hilo rais anajaribu kuzua jambo ambalo halitakiwi kutumiwa kwa sasa, amesema Nancy Pelosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.