Pata taarifa kuu
HAITI-MAANDAMANO-SIASA

Haiti yaendelea kukumbwa na maandamano, rais aonya

Hatimaye rais wa Haiti Jovenel Moise amevunja ukimya, baada ya wiki kadhaa za vurugu nchini mwake. Wakati maandamano yakiendelea kwa siku ya nane, maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana wakiomba rais Moise ajiuzulu.

Maandamano katikati ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, Februari 12, 2019.
Maandamano katikati ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, Februari 12, 2019. HECTOR RETAMAL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Jovenel Moise amefutilia ombi hilo na kusema kuwa atahakikisha amemaliza muhula wake wa miaka mitano.

Msimamo huo wa rais Moise umewashangaza wengi nchini Haiti. Katika hotuba aliyotoa Alhamisi, Februari 14 kwenye televisheni ya serikali, rais Moise amekumbusha kuwa serikali za mpito zilikuepo kabla ya utawala wake na kwamba, maneno hayo, ndiyo "yalisababisha kutokea kwa machafuko na umwagaji damu nchini Haiti". Ameongeza kuwa "mabadiliko, nchi kukosa utulivu na biashara ya madawa ya kulevya vina uhusiano wa karibu".

Jovenel Moise ametoa mifano mingi inayohusiana na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya. Kauli yake hiyo inakuja siku moja baada ya maandamano makubwa kufanyika katikati mwa mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince. Mmoja wa viongozi wakuu wa makundi ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya alionekana hadharani na watu wake wakibebelea silaha bila hofu yoyote.

Wakati huo huo kulitokea urushianaji risasi kati ya baadhi ya waandamanaji na maafisa wa polisi katika mtaani karibu na ofisi za rais. Pia, Jovenel Moise ameonya kuwa "kamwe hatokabidhi nchi kwa makundi ya watu wenye silaha na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.