Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Venezuela: Tani 30 za msaada wa kibinadamu zazuiliwa kwenye mpaka

Msaada wa kibinadamu kwa Venezuela umendelea kukusanywa nchini Colombia ambapo tani thelathini za chakula na dawa zimezuiliwa kwenye mpaka wa Venezuela. Marekani ndio inafadhili na kuendesha shughuli hiyo, kwa makubaliano na Colombia na upinzani nchini Venezuela.

Raia huyu wa Venezuela anabebelea bango ambalo limeandikwa "tunahitaji msaada wa kibinadamu kwa sasa" huko Cucuta, mji ulio kwenye mpaka kati ya Colombia na Venezuela, Februari 6, 2019.
Raia huyu wa Venezuela anabebelea bango ambalo limeandikwa "tunahitaji msaada wa kibinadamu kwa sasa" huko Cucuta, mji ulio kwenye mpaka kati ya Colombia na Venezuela, Februari 6, 2019. REUTERS/Luisa Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Juan Guaido aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela, alimwomba Rais Maduro kutozuia msaada huo baada ya jeshi kufunga daraja kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Hivi ni vita vipya vinavyozuka nchini Venezuela. Marekani, Canada, na Umoja wa Ulaya wametoa zaidi ya dola milioni 65 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu nchini Venezuela. Msaada ambao kwa sasa umewasili nchini Colombia, lakini serikali ya Venezuela imefunga madaraja kadhaa ili kuzuia kuvuka mpaka, anasema mwandishi wetu huko Caracas, Benjamin Delille.

"Tunahitaji msaada huo. Watu wanauhitaji kwa kweli. Kwa kweli raia hapa tunakabiliwa na ukosefu wa chakula, hasa dawa. Lakini nadhani hawataruhusu msaada huo kuingia nchini Venezuela, " amesema Jose Manuel, mkaazi wa kijiji cha Petare, nchini Venezuela.Wafuasi wengi wa Nicolas Maduro wanaona msaada huo kama kama shinikizo dhidi ya rais wao

"Nadhani ni hatua ya nchi za Amerika Kaskazini kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela. Hatuhitaji msaada wa kibinadamu. Hatuutaki kabisa, hatukumuomba msaada mtu yeyote. Tunachotaka watuache tuishi kwa amani, watuache tufanye kazi. Sisi ni waathirika wa vita vya kiuchumi, hata kama watu wengine wanakataa. Na kwa njia ya vita hii ya kiuchumi, walituibia haki ya kuwa na chakula. "

Raia wa Venezuela wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, huku mdororo wa kiuchumi ukiendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.