Pata taarifa kuu
VENEZUELA- MAANDAMANO-SIASA

Maelfu wamiminika mitaani Venezuela kushinikiza jeshi kutomuunga mkono Maduro

Maelfu ya raia nchini Venezuela, wakiongozwa na Spika wa bunge Juan Guaido aliyejitangaza rais wa mpito wameandamana Jumatatu wiki hii ili kushikiza jeshi kutomtii rais Nicolas Maduro."

Upinzani ukiandamana mjini Caracas, Venezuela.
Upinzani ukiandamana mjini Caracas, Venezuela. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

“Msiwapigi risasi watu ambao pia wanatetea familia zao," Juan Guaido,ametoa wito kwa jeshi.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya Nicolas Maduro imeanzisha mbinu mpya ya kukabiliana na kiongozi mkuu wa upinzani, Spika wa bunge la nchi hiyo Juan Guaido, ambaye hivi karibuni amejitangaza kuwa ni rais wa mpito wa Venezuela.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tarek William Saab, mshirika wa karibu wa Nicolas Maduro, ameanzisha uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani. Bw Saab ameomba Mahakama Kuu (TSJ), taasisi iliyo mikononi mwa Nicolas Maduro, kupiga marufuku Juan Guaido kuondoka nchini Venezuela na kuzuia akaunti zake za benki.

Hivi karibuni Bw Guaido alitoa wito wa kufanyika kwa maandamano mapya Jumatano na Jumamosi wiki hii kwa lengo la kushinikiza jeshi, linaloendelea kumtii rais aliyechaguliwa Nicolas Maduro, na kuunga mkono onyo la Ulaya kwa ajili ya uchaguzi huru.

Siku ya Jumamosi nchi sita za Ulaya (Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Ureno, Uholanzi) zilimpa Nicolas Maduro muda wa siku nane kuitisha uchaguzi, la sivyo zitamtambua Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela. Muda huo utatamatika siku ya Jumapili.

Tayari Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini zimetangaza kuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.