Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAREKANI-SIASA

Venezuela yafunga balozi zake Marekani

Venezuela imeingia katika uhasama na Marekani, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba anamuunga mkono Spika wa Bunge Juan Guaido aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela siku ya Jumatano wiki hii.

Rais wa Venezuela Maduro.
Rais wa Venezuela Maduro. Miraflores Palace/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya Marekani imesababisha mvutano wa kidiplomasia na utawala wa Nicolas Maduro ambaye amepata uungwaji mkono wa jeshi la nchi hiyo.

Wakati huo huo Marekani imewataka wafanyakazi wa ubalozi wake wasio kuwa na umuhimu nchini kuondoka nchini Venezuela.

Kwa upande wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonesha kuunga mkono waandamanaji nchini Venezuela dhidi ya rais Nicolas Maduro. Macron ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwa Kifaransa na Kihispania, kwamba kufuatia kuchaguliwa bila uhalali kwa Nicolas Maduro mwezi Mei mwaka 2018, mataifa ya Ulaya yanaunga mkono kurejeshwa kwa demokrasia nchini humo. Macron hakutaja jina la Juan Guaido, kiongozi wa bunge la taifa linalodhibitiwa na upinzani nchini Venezuela ambaye amejitangaza kuwa rais wa mpito.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Federico Mogherini amesema katika taarifa kwamba sauti za watu wa Venezuela zinazodai demokrasia haziwezi kupuuzwa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa mazungumzo na kusema ghasia ama kuchochea ghasia hizo kunapaswa kuepukwa baada ya Marekani , na mataifa mengi ya Amerika kusini kumtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido kuwa rais wa nchi hiyo.

Awali Majenerali wanane ambao wanaongoza Majimbo muhimu ya nchi hiyo walisema bado "wanamtii" Rais Nicolas Maduro, katika ujumbe uliorushwa kwenye televisheni ya serikali.

Waziri wa Ulinzi, Jenerali Vladimir Padrino, alionekana katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii huko Caracas akizungukwa na uongozi wa jeshi katika ngazi ya juu ili kulaani "jaribio la mapinduzi" lililofanywa na Spika wa Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.