Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Venezuela: Jeshi lamuunga mkono Nicolas Maduro

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amepata uungwaji mkono wa jeshi la nchi hiyo siku moja baada ya Spika wa Bunge Juan Guaido kujitangaza rais wa mpito wa Venezuela.

Waziri wa Ulinzi wa Venezuela, Vladimir Padrino Lopez, akizungukwa na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi, katika mkutano na waandishi wa habari Caracas Januari 24, 2019.
Waziri wa Ulinzi wa Venezuela, Vladimir Padrino Lopez, akizungukwa na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi, katika mkutano na waandishi wa habari Caracas Januari 24, 2019. REUTERS/Manaure Quintero
Matangazo ya kibiashara

Tayari Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini zimetangaza kuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela.

Kwa upande wa kimataifa, nchi ndogo zinamuunga mkono Nicolas maduro, ikiwa ni pamoja na China, Uturuki, Mexico na Urusi.

hata hivyo Juan Guaido ameendelea kupokea uungwaji mkono.

Siku ya Alhamisi jioni alitangaza kwamba anataka kuandaa haraka uchaguzi mpya.

Waziri wa Ulinzi, Jenerali Vladimir Padrino, alionekana katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii huko Caracas akizungukwa na uongozi wa jeshi katika ngazi ya juu ili kulaani "jaribio la mapinduzi" lililofanywa na spika wa Bunge.

"Ninatoa tahadhari kwa raia wa Venezuela kwamba jaribio la mapinduzi limefanywa dhidi ya taasisi za uongozi wa nchi, dhidi ya demokrasia, dhidi ya Katiba yetu, dhidi ya Rais Nicolas Maduro, rais wetu halali," alisema waziri huyo.

Awali Majenerali wanane ambao wanaongoza Majimbo muhimu ya nchi hiyo walisema bado "wanamtii" Rais Nicolas Maduro, katika ujumbe uliorushwa kwenye televisheni ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.