Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Marekani: Kaimu waziri wa sheria atangaza kujiuzulu

Kaimu Waziri wa Sheria wa Marekani Rod Rosenstein anatarajiwa kujiuzulu kwenye nafasi yake baada ya William Barr kuthibitishwa kuwa waziri mpya wa sheria.

Kaimu Waziri wa Sheria wa Marekani Rod Rosenstein anatarajia kujiuzulu baada ya kuthibitishwa uteuzi wa William Barr kama waziri mpya wa sheria, vyombo vya habari vya Marekani vimearifu, Januari 9, 2019.
Kaimu Waziri wa Sheria wa Marekani Rod Rosenstein anatarajia kujiuzulu baada ya kuthibitishwa uteuzi wa William Barr kama waziri mpya wa sheria, vyombo vya habari vya Marekani vimearifu, Januari 9, 2019. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rod Rosenstein aliwahi kukagua uchunguzi wa mwendesha mashtaka Mueller katika kesi ya Urusi kuingilia katika kampeni za uchaguzi wa urais nchini Marekani. Mara nyingi alikosolewa na Donald Trump. Kuondoka kwa Rod Rosenstein itakuwa ni furaha kwa rais Donald Trump.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu huko Washington, Anne Corpet, Donald Trump mara kwa mara amekuwa akimkosoa Rod Rosenstein. Rais Trump alikwenda mbali hadi kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Twitter inayomuonyesha Rod Rosenstein akiwa kizimbani, pamoja na mwendesha mashitaka Mueller.

Wakati Jeff Sessions alikuwa bado waziri wa sheria, Rod Rosenstein alikuwa naimbu wake, na yeye ndiye alikuwa akindesha uchunguzi katika kesi ya Urusi kuingilia kampeni za uchaguzi wa Marekani.

Tangu kujiuzulu kwa Jeff Sessions, Rod Rosenstein ambaye rasmi alikaimu nafasi hiyo aliendelea kukaguwa kazi ya Mwanasheria Mueller.

Hata hivyo Rod Rosenstein anaendelea kuhusishwa katika uchunguzi huo unaoendeshwa kila siku.

Tangazo la kujiuzulu kwake liliibua wasiwasi kuhusu hatima ya baadaye ya mwendesha mashitaka. Kikao cha baraza la Seneti cha kumthibitisha waziri mpya wa sheria William Barr kimepangwa kufanyika Jumanne ya wiki ijayo.Bila shaka Wademocrats watataka kupata uhakikisho kuhusu swala hilo.

Lindsey Graham, Seneta kutoka chama cha Republican ambaye yuko karibu na Donald Trump, hata hivyo, amesema waziri mpya wa sheria hana nia mbaya ya kuzuia kazi ya mwendesha mashitaka.

"Ninawahakikishia kwamba William Barr atakuwa msaidizi wa Robert Mueller na kwamba atakuwa tayari kumruhusu amalize kazi yake," amesema Seneta Graham.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.