Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 09/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 09/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Trump aomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na Mexico

media Rais Donald Trump wakati wa hotuba yake kwa taifa, Jumatatu, katika ikulu ya White House. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani, Donald Trump ametaka kupewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta mrefu kwenye mpaka wa nchi hiyo na Mexico, akisema ukuta huo utasaidia kupunguza hali tete ya kibinadamu na kuimarisha usalama.

Akihutubia taifa kupitia televisheni rais Trump amewakashifu wabunge wa Democrats kwa kuendelea kukwamisha mpango wake, akiwaita wasaliti waliotayari kuona wananchi wa taifa hilo wakiendelea kutaabika.

Saa chache baada ya hotuba yake, viongozi wa Democrats wamejitokeza na kumkosoa vikali rais Trump wakimtaka afungue shughuli za Serikali mapema iwezekanavyo.

Rais Donald Trump ameapa kuendelea na mipango yake ya kujenga ukuta wa urefu wa kilomita 3000 kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Ukuta huo utakuwa na urefu wa kati ya mita 9 na 16 na utajengwa kwa kutumia changarawe.

Warepublican na wafuasi wao wanasema kuwa ukuta huo utawazui raia wa Mexico wanaoingia Marekani kinyume na sheria.

Mpaka kati ya Marekana na Mexico una umbali wa kilomita 3000.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana