Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Maduro kutawazwa Alhamisi kama rais wa Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro anatarajiwa kuapishwa Alhamisi wiki hii Januari 10, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, wa miaka sita. Nicolas Maduro alishinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 68 ya kura nchini Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro. REUTERS/Marco Bello
Matangazo ya kibiashara

Maduro mwenye umri wa miaka 56, ataapishwa na Jaji wa Mahakama ya Juu, katika nchi ambayo bunge linadhibitiwa na wapinzani.

Marekani, Umoja wa nchi za Amerika na Umoja wa Ulaya, zimesema hazimtambua Maduro kama kiongozi halali wa nchi hiyo, na wamekuwa wakishinikiza uchaguzi mpya.

Hata hivyo, anaiungwa mkono na Urusi, China na Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.