Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Nancy Pelosi achaguliwa kuwa Spika wa bunge la wawakilishi Marekani

Hatimaye Bi Nancy Pelosi wa chama cha Demokratic amechaguliwa kuwa spika wa kwanza mwanamke wadhifa mkubwa kabisa katika bunge la Marekani.

"Haijalishi muda itakaochukuwa, wala mara watakazoulizwa, jibu litabakia kuwa hapana kwa ujenzi wa ukuta, " Bi Pelosi amesema katika mahojiano na shirika la habari la NBC la nchini Marekani.
"Haijalishi muda itakaochukuwa, wala mara watakazoulizwa, jibu litabakia kuwa hapana kwa ujenzi wa ukuta, " Bi Pelosi amesema katika mahojiano na shirika la habari la NBC la nchini Marekani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa rais wa Marekani Donald Trump umeendelea kupata pigo kubwa baada ya taarifa za vyombo vya habari vya Marekani kutangaza kwamba chama cha Demokratic kimepata ushindi baraza la Seneti.

Hii ina maana rais Trump sasa atakabiliwa na changamoto mpya na nzito wakati huu akilitaka baraza la seneti kukubali kupitisha azimio lake la kutaka kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Sikua ya Jumatano Donald Trump alionyesha umuhimu wa ukuta anaotaka kujenga kwenye mpaka na Mexico, Lakini wapinzani wake wa Democrats wamekataa katu katu kufadhili mradi huo.

Uteuzi huu wa Nancy Pelosi unakuja shughuli za serikali zinaendelea kukwama nchini Marekani.

Siku ya Jumatano mazungumzo kati ya Rais Donald Trump na wakuu wa vyama bungeni, yaliambulia patupu mjini Washington.

Kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico ilikuwa ahadi muhimu ya kampeni ya Rais Trump, na kulingana na afisa mmoja wa Ikulu ya White House aliyenukuliwa na shirika la habari la Associted Press, amethibitisha kuwa Trump katika kikao na viongozi wa vyama, alitamka kwamba hawezi kuachana na azma ya kuujenga ukuta huo, kwa sababu akifanya hivyo ataonekana mjinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.