Pata taarifa kuu
BRAZIL-RAIS-MPYA-JAIR

Rais mpya wa Brazil aapishwa, aahidi mabadiliko makubwa

Jair Bolsonaro ameapishwa kuwa rais mpya wa Brazil katika sherehe zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa taifa hilo jijini Brasilia, wakiwemo viongozi wa mataifa mbalimbali duniani.

Rais mpya wa Brazil  Jair Bolsonaro, baada ya kuapishwa jijini  Brasília, Januari 1 2019.
Rais mpya wa Brazil Jair Bolsonaro, baada ya kuapishwa jijini Brasília, Januari 1 2019. REUTERS/Ricardo Moraes
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Bolsonaro kushinda Uchaguzi wa urais mwezi Oktoba mwaka 2018.

Rais huyo mpya, ameahiidi  kuijenga Brazil mpya , itakayoimarika bila ubaguzi na mgawanyiko.

Aidha, rais huyo wa 38 ambaye pia aliwahi kuwa mwanajeshi amesema matamanio yake ni kuunda muungano wa pamoja wa kisiasa utakaomsaidia kupambana na ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma na kuhakikisha kuwa nchi hiyo inakuwa salama.

Licha ya ahadi hizi, wapinzani wake bado wanamwona kama kiongozi mbaguzi kwa sababu ya msimamo wake wa kupinga mapenzi na ndoa ya jinsia moja, utoaji mimba na sera ya usawa wa jinsia katika maeneo ya uteuzi na uwakilishi.

Rais wa Marekani amempongeza kwa hotuba aliyotoa, na kusema nchi yake iko pamoja naye.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, mwenzake wa Hungary Viktor Orban ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria kuapishwa kwa rais Bolsonaro.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.