Pata taarifa kuu
MAREKANI-WAHAMIAJI-USALAMA

Marekani yachukua hatua ya kuzuia mipaka yake dhidi ya wahamiaji haramu

Nchi ya Marekani imesema haitaruhusu tena watu wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria kuomba hifadhi, tangazo linalokuja baada ya rais Donald Trump kutia saini sheria tata ya kukabiliana na wahamiaji.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi vya kuomba hifadhi vinaelezwa na maofisa wa juu wa Marekani kuwa vinalenga kumaliza ukiukwaji wa sheria wa kihistoria katika mfumo wa uhamiaji nchini humo na hasa kwenye mpaka wa nchi hiyo na Mexico.

Uamuzi huu wa Serikali uliochapishwa kwenye tovuti ya wizara ya mambo ya nje, tayari umezua mjadala mkali kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu, ambayo yanasema haki ya kuomba hifadhi nchini humo ni ya kila mtu bila kujali namna alivyoingia.

Licha ya wanasheria kudai kuwa rais hana mamlaka ya kubatilisha sheria hiyo, utawala wa rais Trump wenyewe umesisitiza kuhusu mamlaka aliyonayo rais na kwamba hatua hii inachukuliwa kwa maslahi ya usalama wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.