Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-USALAMA-WAHAMIAJI

Askari zaidi ya 5,000 wa Marekani watumwa kwenye mpaka na Mexico

Marekani imetuma jeshi lake kwenye mpaka na Mexico. Hatua hiyo inakuja wakati maelfu ya wahamiaji kutoka Amerika ya Kati, wakijaribu kuingia nchini Marekani.

Mpaka wa Marekani na Mexico huko Nogales, Arizona.
Mpaka wa Marekani na Mexico huko Nogales, Arizona. REUTERS/Adrees Latif
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi imetangaza kutuma askari 5,200, ambao watajiunga na wengine na kufikia waliotumwa na kufikia idadi ya 19,000. Hatua iimechukuliwa baada ya hotuba ya Rais Donald Trump, wiki moja kabla ya uchaguzi wa nusu muhula.

Tangu mapema Jumatatu asubuhi , Donald Trump alijaribu kuweka kuweka suala hili la wahamiaji kwenye mjadala. Katika ukurasa wake wa Twitter, alielezea msafara wa wahamiaji hao kama kitendo cha "uvamizi," akiongeza kuwa "wahalifu wengi" wamejipenyeza kwenye msafara huo.

Rais Trump amesema utawala wake umeanza kuchukua hatua. Jenerali Terrence O'Shaughnessy amesema "Ifikapo mwishoni mwa wiki, tutatumia askari zaidi ya 5,200, ambaomwatajiunga na wengine 2,090 wa kikosi cha ulinzi wa taifa ambao walitumwa mapema kwenye mpaka na Mexico. Usalama wa mipaka ni ulinzi wa nchi. Na jeshi la Marekani litasaidia kitengo hicho kinachohusika na suala hili ili kuimarisha kulinda mpaka wetu. "

Ili kukabiliana na misafara miwili ambayo kila mmoja unajumuisha wahamiaji 3,000 hadi 4,000, ambao wengi wao ni wanawake na watoto, jeshi la Marekani limetuma idadi kubwa ya askari sawa na ile ilioko nchini Syria na Iraq.

Lakini jeshi litakuwa na uwezo mdogo, watasaidia hasa maafisa 16,500 wa polisi inayohusika na kulinda mipaka. Helikopta zao na ndege zilizotengenezwa kwa teknolojia ya juu zitasaidia kuwakamata wahamiaji, hata wakati wa usiku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.