Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFRIKA-BILIONEA-MICROSOFT

Bilionea wa Marekani aliyelipenda bara la Afrika Paul Allen, afariki dunia

Paul Allen, mmoja wa waanzalishi wa Microsoft mwaka 1975, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65, baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa lymphoma unaoathiri damu.

Bilionea wa Marekani Paul Allen aliyefariki duniani Oktoba 15 2018
Bilionea wa Marekani Paul Allen aliyefariki duniani Oktoba 15 2018 Mandatory Credit: Mark J. Rebilas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema hali ya Bilionea huyo ilibadilika ghafla wiki mbili zilizopita, alipoonekana amepata nafuu baada ya kutibiwa mwaka 2009, na hata Madaktari wake walikuwa na imani kuwa afya yake imeimarika.

Allen, alianzisha Microsoft akiwa na mshirika wake tajiri Bill Gates ambaye amesema amesikitishwa sana na kifo cha rafiki yake.

“Nimevunjika moyo sana kwa kupata taarifa za kufariki dunia kwa rafiki yangu wa karibu, singeweza kufanikiwa bila ya uwepo wake,” amesema Gates.

Aidha, Gates amesema kuwa Allen, alistahili kuendelea kuwepo kwa muda zaida kwa sababu ya mchango wake mkubwa katika masuala ya teknolojia ambayo yameibadilisha dunia.

Mbali na teknolojia, Allen alikuwa rafiki mkubwa wa mataifa ya bara la Afrika, kwa kutumia fedha zake kufadhili miradi mbali mbali ikiwemo ya kuhifadhi Wanyamapori.

Miaka ya 1970, alitoa Dola Milioni 7 kusaidia katika uhesabuji wa ndovu katika mataifa zaidi ya 20 barani Afrika kwa lengo la kupata idadi kamili ya Wanyama hao wanaovutia watalii na wanaolengwa.

Amekuwa akifadhili pia uzalishaji wa umeme nchini Kenya, kwa lengo la kuongeza kiwango cha umeme kuwasaidia raia wa kawaida lakini pia wafanyibiashara wadogo wadogo.

Mwaka 2014, alitoa Dola Milioni 100 kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya Ebola katika mataifa ya bara la Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.