Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga hatari Michael chaelekea Georgia na Alabama

Jimbo la Florida linashuhudia kimbuga kikubwa kuwahi kutokea hasa, Kaskazini Magharibi mwa jimbo hilo. Upepo mkali umeshuhudiwa lakini pia miji imejaa maji, miti imeangukia makaazi ya watu na maeneo ya biashara kuharibika.

Uharibifu mkubwa uliofanywa na kimbunga Michael Florida.
Uharibifu mkubwa uliofanywa na kimbunga Michael Florida. JOE RAEDLE / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kimbuga hiki kimepewa jina la Michael. Maafisa wanasema mtu mmoja amepoteza maisha kutokana na janga hili.

Watu wapatao 375,000 wanaoishi katika ukanda wa pwani wa Jimbo la Florida wametakiwa kuyahama makazi yao ili kuepusha madhara.

Kwa mujibu wa kituo kinachohusika na masuala ya vimbunga nchini Marekani (NHC), madhara ya kimbunga Michael yatakuwa makubwa na ambayo hayajawahi kutokea katika baadhi ya maeneo.

Hata hivyo Kimbunga Maichael kinatarajia kupiga maeneo ya Georgia na Alabama Alhamisi hii jioni, kwa mujibu wa NHC.

Taarifa za watabiri wa hali ya hewa zimesema kuwa kimbunga hicho kwa sasa kimeingia katika hatua ya tatu na kuongezeka kasi yake kwa kadri kinavyopitia ghuba ya Mexico kuelekea Majimbo ya Alabama na Georgia.

Kutokana na hali hiyo majimbo ya Alabama, Florida na Georgia yametangaza hali ya hatari, ambapo Alabama maeneo 92 ya watu wake wanatakiwa kupisha madhara ya kimbunga hicho Michael kusini mwa jimbo la Georgia na maeneo 35 ya jimbo la Georgia kimbuka hicho kinatarajiwa kuyafikia.

Naye Gavana wa Jimbo la Carolina Kaskazini, Roy Cooper ameonya kwamba watu wake wanatakiwa kuchukua tahadhari kwani huenda madhara ya kimbunga hicho yakawa makubwa zaidi ya Kimbunga Florence kilicholikumba eneo hilo mwezi uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.