Jaji Kavanaugh amekula kiapo katika sherehe iliyofanyika kwenye ikulu ya White House siku ya Jumatatu. Aliahidi kuwa kutumikia taifa bila kuwa na "upendeleo".
"Mahakama Kuu ni taasisi ya sheria. Sio taasisi ya kisiasa au ya upendeleo fulani. Ni timu ya majaji tisa na mimi niko tayari kutoa ushiriki wangu kwa timu hiyo, "aliahidi.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald amemuomba radhi kwa niaba ya raia wa Marekani Jaji Brett Kavanaugh kwa kile alichodai kuwa ni kampeni chafu za kisiasa zilizolenga kuharibu sifa binafsi ya Brett kutokana na mambo ya uzushi na uongo.
Hata hivyo bado Wanasheria wakuu wa chama cha upinzani hawakubaliani na uteuzi wa Bw Brett ambaye wanamtuhumu kwamba ana makosa mengi ya kinidhamu likiwemo lile la madai ya kutaka kumbaka aliyekuwa mwanafunzi mwezake Christine Blasey enzi hizo wakisoma sekondari na kwamba wanataka kuyafikisha upya madai hayo kwa FBI.