sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Hukumu dhidi ya mcheshi nguli Bill Cosby yazua mjadala Marekani

media Mcheshi nguli na mwigizaji maarufu Bill Cosby, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 hadi 10 kwa kosa la unyanyasaji wa kimapenzi, Septemba 25, 2018. Courtesy Montgomery County Correctional Facility/via REUTERS

Mwigizaji maarufu na mkongwe nchini Marekani, Bill Cosby amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi kumi jela, baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuwadhalilisha kingono wanawake zaidi 60 miaka 14 iliyopita.

Cosby aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka kadha yaliyotokana na madai ya wanawake wengi alikutwa na hatia mwezi Aprili mwaka huu katika makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono kwa kumpa dawa na kumfanyia tendo la ngono Andrea Constand mwaka 2004.

Cosby mwenye umri wa miaka 81, alikuwa akitajwa na mashabiki wake kama baba wa Marekani na hukumu yake imeleta mgawanyiko wa mawazo, baadhi wakienda mbali zaidi na kuingiza dhana ya ubaguzi wa rangi.

Cosby kwa mara ya kwanza alikutwa na hatia mwezi April mwaka huu na siku ya Jumanne wiki hii baraza la wazee wa mahakama kwa kauli moja waliridhia kumtia hatiani Cosby na kumuhukumu kifungo jela.

Mawakili watetezi wa Cosby, mwenye umri wa miaka 81, walionyesha dalili awali kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana