Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Canada yataka kufuta mkataba wa silaha wa dola biloni 15 na Riyadh (Justin Trudeau)
Amerika

Marekani yaionya Iran kwa mara nyingine

media Askari waliouawa na wengine kujeuhiwa kufuatia mashambulizi dhidi ya gwaride la wanajeshi huko Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, Septemba 22, 2018. ALIREZA MOHAMMADI / ISNA / AFP

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley ameitaka nchi ya Iran kujitazama kwanza kwa kusababisha shambulio la mwishoni mwa juma ambalo lilisababisha vifo vya watu 25 wakiwemo raia wa kawaida na wanajeshi.

Matamshi ya Haley yamekuja siku chache tu baada ya utawala wa Tehran kuituhumu Marekani na washirika wake kufadhili makundi ya kigaidi yaliyotekeleza shambulio la mwishoni mwa juma.

Akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni nchini Marekani cha ABS Haley amesema akisisitiza kutohusika kwa nchi yake na kuitaka Iran kuacha kutafuta mchawi.

Nchi hizo mbili kwa miongo kadhaa zimekuwa katika uhusiano mbaya ambapo Marekani imekuwa ikiilaumu Iran kwa kwa kuzalisha silaha za kinyuklia jambo ambalo Iran imekuwa ikilakanusha ziku zote.

Matamshi ya Marekani yanakuja wakati siku ya Jumanne wakuu wa nchi kutoka mataifa mbalimbali duniani watahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa huku ajenda ya Iran na Korea Kaskazini zikitarajiwa kutawala mkutano huu wa mwaka.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana