Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAJANGA YA ASILI

Maelfu ya watu watoroka makazi yao Marekani kufuatia kumbunga Florence

Rais Donald Trump ametangaza hali ya hatari katika maeneo ya Kaskazini na kusini mwa jimbo la Carolina ambapo pia eneo kubwa la Washington DC limechukua pia tahadhari kufuatia kimbunga Florence.

Wafanyakazi waweka vifaa vyenye nguvu kwenye madirisha ya duka huko Wilmington, Carolina Kusini kabla ya kuwasili kwa kimbunga Florence.
Wafanyakazi waweka vifaa vyenye nguvu kwenye madirisha ya duka huko Wilmington, Carolina Kusini kabla ya kuwasili kwa kimbunga Florence. ©REUTERS/Chris Keane
Matangazo ya kibiashara

Takribani watu milioni 1.7 wanayahama maeneo yao kwa hiari na wengine kwa amri maalumu ili kuepuka madhara ya kimbunga hicho.

Kimbunga hicho kinasafiri kwa kilomita 195 kwa saa,huku mawimbi yake yakienda juu kimo cha mita 25.

Kimbunga Florence kinachotajwa kibaya kuwahi kutokea siku ya ijumaa kinatarajiwa kuyapiga maeneo ya pwani ya mashariki.

Kwa mujibu wa chanzo cha usalama nchini Marekani kwa sasa kuna msongamano wa magari barabarani, baada ya zaidi ya watu milioni moja kuamriwa kuyahama makazi yao.

Majimbo kadhaa nchini Marekani yametangaza hali ya hatari kufuatia kimbunga Florence kudaiwa kuelekea pwani ya mashariki mwa taifa hilo.

Kimbuga hicho kimepewa jina Florence na wakazi wa jimbo hilo wameambiwa kukimbilia maeneo salama.

Upepo mkali, ukiandamana na mafuruko makubwa yanatarajiwa kuharibu miundombinu na kutishia maisha ya wakazi wa eneo hilo ambalo linapatikana Mashariki mwa Pwani ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.