Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Serikali mpya ya Bolivia yamtambua Guaido kama rais wa Venezuela (waziri)
Amerika

Moto mkubwa wateketeza moja ya Makumbusho kongwe ya taifa Brazil

media Afisa wa polisi atoa ulinzi kando ya Makumbusho ya Taifa ya Rio, iliyovamiwa na moto Septemba 3, 2018. REUTERS/Ricardo Moraes

Moto mkubwa umeteketeza Makumbusho ya taifa ya Rio de Janeiro, mojawapo ya makumbusho kongwe zaidi nchini Brazil. Mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo au majeruhi. "Leo ni siku mbaya nchini Brazil," amesema Rais wa nchi hiyo Michel Temer.

Moto, huo ambao ulitokea Jumapili wiki hii, chanzo chake bado haukijulikani, ulianza karibu saa moja usiku1 (saa za Brazil, wakati Makumbusho ya taifa ya Rio de Janeiro ilikua imefungwa kwa umma, vyombo vya habari kadhaa vya Brazil vimeripoti. "Mpaka sasa, hakuna taarifa za vifo au majeruhi. Moto ulisambaa haraka sana. Kuna vitu vingi vya kushika moto haraka katika makumbusho, "amesema msemaji wa kikosi cha Zima Moto cha Rio de Janeiro.

Chanzo cha moto bado kinachunguzwa na mamlaka nchini Brazil. Mapema mwaka huu Makumbusho hiyo ilisherekea kutimiza miaka 200.

Kwa mujibu wa tovuti ya makumbusho, Ndani ya makumbusho kulikua na vitu mbalimbali vya Historia ya Brazil na nchi nyingine ikiwemo Misri.

Picha ya Globo televisheni inaonyesha jengo kubwa la mita 13,000-mraba upande wa kaskazini mwa Rio de Janeiro, ikiteketea kwa moto mkubwa kwa muda wa saa kadhaa. Licha ya kupelekwa haraka kwa maafisa wa kikosi cha Zima Moto, moto ulivamia mamia ya vyumba katika makumbusho, na kuteketeza kila kitu. Baada ya masaa zaidi ya tatu na nusu, maafisa wa kikosi cha Zima Moto hawajafaulu kudhibiti moto huo.

"Miaka mia mbili ya ujuzi yatoweka"

"Leo ni siku mbaya kwa Brazil. Miaka mia mbili ya kazi, utafiti na ujuzi yatoweka, "amesema Rais Michel Temer katika katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Naibu mkurugenzi wa makumbusho, Luiz Fernando Dias Duarte, amesema "nina huzuni mkubwa, nimekata tamaa " na "nina hasira kubwa". "Nyaraka zote za kihistoria, zilizohifadhiwa katika eneo la katikati ya jengo, zimeteetea kwa moto," amesema.

Hakuna msaada kutoka kwa mamlaka

Dias Duarte ameshtumu mamlaka nchini Brazil kwa "kutokua na umakini" na amebaini kwamba hakuona "msaada wowote mkubwa na wa haraka" kwa kukabiliana na moto huo dhidi Makumbusho hiyo, makazi ya zamani ya familia ya kifalme.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana