Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Mwanasheria mkuu wa Marekani amuonya Trump

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions amesema, hataruhusu mashambulizi ya kisiasa kutoka kwa rais Donald Trump yaathiri kazi katika Ofisi yake. Trump amesema hivi karibuni kuwa, Bwana Sessions, ameshindwa kuwajibika ipasavyo kazini.

Rais Donald Trump na Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions huko Washington, Marekani, Mei 15, 2017.
Rais Donald Trump na Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions huko Washington, Marekani, Mei 15, 2017. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria huyo ameendelea na uchunguzi wa kina kubaini iwapo Urusi iliingia Uchaguzi wa wakwa 2016 na kumsaidia Trump kushinda.

Wakati huo huo, Trump ameonya kuwa iwapo kutakuwa na jaribio lolote la kumwondoa madarakani, uchumi wa Marekani utatikisika.

Trump ameendelea kukabiliwa na ukosoaji mkubwa ndani na nje ya Marekani

Hivi karibuni Rais Donald Trump alipata pigo kubwa mara mbili katika kesi mbili ambazo anaonekana kuhusika. Jumanne wiki hii, Paulo Manafort, meneja wake wa zamani wa kampeni, alipatikana na hatia ya udanganyifu wa kodi na masuala ya kibenki kwa mashtaka nane kati ya 18 yanayomkabili.

Wakati huo huo Michael Cohen, wakili wa zamani wa Donald Trump, alikiri mashtaka nane, sita ya udanganyifu wa kodi na benki na mashitaka mawili yanayohusiana na kufadhili kampeni ya uchaguzi kinyume cha sheria. Mbaya zaidi, mwanasheria wa zamani wa rais alihakikishia mahakamani kuwa alikiuka sheria kwa ombi la rais.

Hili ni pigo kubwa kwa rais wa Marekani baada ya kuhusihwa na mtu ambaye alikua akimuamini kwa zaidi ya muongo mmoja. Michael Cohen alieleza mwenyewe kuwa ni mtu wa karibu wa Donald Trump. Alisema kuwa alikuwa akihusika na kutatua matatizo yake. Lakini mwanasheria huyo wa zamani wa rais Trump sasa anaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa kwa Donald Trump.

Mbele ya Mahakama, Michael Cohen alidai alilipa dola 130,000 na 150,000 kwa wanawake wawili ili kuwaziba midomo kuhusu mahusiano yao na Donald Trump kwa ombi la Donald Trump kwa lengo la kushawishi uchaguzi.

Laikini Rais Donald Trump alipuuzia mbali madai hayo ya Bw Cohen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.