Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Iván Duque: Ninapanga kuliunganisha taifa letu lililogawanyika

media Ivan Duque ametawazwa kuwa rais wa Colombia kwa muhula wa miaka minne,Jumanne Agosti 7, 2018 huko Bogota. Fabian Ortiz/Courtesy of Colombian Presidency/Handout via REUTER

Rais mpya wa Colombia Iván Duque, ambaye anatajwa kuwa mdogo zaidi kuwahi kutawala taifa hilo, amepiashwa na kuanza kuongoza taifa hilo la Amerika Kusini.

Rais huyo mpya anamrithi rais aliyemaliza muda wake Juan Manuel Santos, baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu mwezi Juni.

Akiwahotubia raia wa Colombia kwa mara ya kwanza akiwa rais , Duque ameahidi kuliunganisha taifa hilo na kuimarisha hali ya uchumi.

Aidha, Wakili huyo wa zamani ameahidi kupambana na ufisadi na wale wanaofanya makosa ya kuhujumu uchumi.

Pamoja na hayo yote, kiongozi mpya amewaambia raia wa nchi hiyo kuwa ana nia ya kuufanyia marekebisho mkataba wa amani uliofikiwa kati ya serikali iliyopita na waasi wa FARC.

Tangu mkataba huo mwaka 2016, FARC kimekuwa chama cha kisiasa na kinawakilishwa bungeni.

Rais wa zamni Santos amemtaka rais huyu mpya kuheshimu mkataba huo wa amani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana