Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA-AJALI

Themanini na tano wajeruhiwa baada ya ndege kuanguka Mexico

Watu temanini na tano wamejeruhiwa baada ya ndege iliyokua imebebea abiria 103 kuanguka muda mfupi baada ya kupaa angani nchini Mexico, mamlaka ya uwanja wa ndege Mexico imesema.

Eneo ambako ndege ya shirika la ndege la  Aeromexico. Embraer 190, iliangukia.
Eneo ambako ndege ya shirika la ndege la Aeromexico. Embraer 190, iliangukia. REUTERS/Proteccion Civil Durango
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ya Embraer ya shirika la ndege la Aeromexico ilianguka usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii.

Ndege hiyo yenye chapa 2431 ilikuwa ikifanya safari kati ya Durango, kaskazini mwa nchi na mji mkuu Mexico, shirika la ndege la Aeromexico imebaini kwenye akaunti yake ya Twitter.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Durango, Grupo Aeroportuario Centro Norte, imesema kuwa uchunguzi wa kwanza unaonyesha kuwa ajali hiyo ilitokana na hali mbaya ya hali ya hewa, na kusababisha ndege hiyo kuanguka ghafla.

Gavana wa Jimbo la Durango José Rosas Aispuro amesema katikaa mkutano na waandishi wa habari kwamba upepo mkali ulisababisha ndege hiyo kukosa muelekeo na kupoteza barabara yake ya kawaida kabla kuanguka muda mfupi baada ya ya kupaa angani.

Msemaji wa kikosi kinachokabiliana na majanga dhidi ya raia katika jimbo la Durango, Alejandro Cardoza, amesema mtu mmoja amefariki dunia na wengine 85 wamejeruhiwa, ambapo 37 wamelazwa hospitalini.

Wizara ya afya katika Jimbo la Durango imesema wawili kati ya waliiojeruhiwa wako katika hali mbaya.

Abiria wengi waliondoka peke yao katika ndege hiyo, ameongeza Alejandro Cardoza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.