Msemaji wa Ikulu ya Washingto Donald Trump Sarah Sanders ameiandika Taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter, wakati huu kukiwa na ukosoaji mkubwa kuhusu mkutano wa viopngozi hao wawili uliofanyika siku ya Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Finland, Helsinki.
Sanders amesema majadiliano kuhusiana na ziara hiyo tayari yameanza na kila kitu kimeandaliwa kufanikisha ziara hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa nchini Marekani wameipokea taarifa hiyo shingo upande, miongoni mwao ni mwanasiasa anayeongoza maseneta wa chama cha Democrat nchini humo, Chuck Schumer, ambaye amepinga mualiko huo.
Wanasiasa hao wamesema rais Trump hapaswi tena kukutana ana kwa ana na rais Putin kabla ya kutoa ufafanuzi kuhusu nini kilitokea katika mkutano wake na Putin huko Helsinki.