Pata taarifa kuu
MAREKANI-USURI-USHIRIKIANO

Trump azua sintofahamu katika chama chake kwa kuitetea Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump ameitetea Urusi, na kusema haikuingilia kwa namna yoyote ile Uchaguzi wa urais mwaka 2016 na kumsaidia kupata ushindi.

Donald Trump na Vladimir Putin kwenye mkutano wao na waandishi wa habari, Julai 16, 2018 huko Helsinki.
Donald Trump na Vladimir Putin kwenye mkutano wao na waandishi wa habari, Julai 16, 2018 huko Helsinki. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Kuali ya Trump, inatofautiana na taarifa ya maafisa wa Inteljensia wa Marekani ambao wameendelea kusisitiza kuwa, Urusi iliingilia Uchaguzi huo.

Trump ambaye amekutana na rais Putin jijini Helsinki nchini Finland, amesema anaamini Urusi haikuwa na sababu yoyote ya kuingilia Uchaguzi huo.

Wakuu wa chama cha Trump wakiongozwa na Spika wa bunge la Congress Paul Ryan, wamekosoa kauli ya Trump huku Seneta John MacCain akisema Trump alitoa kauli za aibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.