Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Watu watano wauawa katika majengo ya gazeti la Annapolis

media Maafisa wa polisi wakiwa karibu na majengo ya gazeti la Annapolis ambapo watu watan wameuawa kwa shambulio la risasi. REUTERS/Greg Savoy

Watu watano wameuawa kwa kupigwa risasi katika majengo ya gazeti la Capital Gazette huko Annapolis, Maryland, nchini Marekani. Mtuhumiwa anahojiwa na polisi wa Kaunti.

Kwa mujibu wa Sun Baltimore, mmiliki wa Capital Gazette tangu mwaka 2014, tukio hilo lilitokea saa 2:40 usiku. Watu watano wameuawa na wengine wawili waejeruhiwa, kulingana na ripoti iliyotolewa na Bill Krampf, kaimu Mkuu wa polisi, mbele ya waandishi wa habari. Tukio hilo ni "shambulizi lililolenga gazeti la Capital Gazette," Bill Krampf amesema, akiongeza kuwa gazeti hilo limekua likipokea vitisho kwenye mitandao ya kijamii.

Mtuhumiwa amekamatwa na anahojiwa na polisi, amesema Steven R. Schuh, kiongozi wa Kaunti ya Anne Arundel. Wafanyakazi wa gazeti hilo wanasema mshambuliaji huyo ambaye ni mzungu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 ambaye alijiharibu vidole vyake ili kuepusha kutambulika kwa alama za vidole alifyatua risasi hovyo kupitia mlango wa vioo.

Kupitia mtandao wa twiter wanahabari kadhaa waliokuwa katika ofisi hiyo akiwemo Jimmy DeButts ambaye ni mhariri mkuu katika kampuni ya Capital Gazette wameelezea masikitiko yao kufuatia vifo vya wenzao huku wengine wakisema kwamba walikuwa ni kama ndugu zao.

Ikulu ya White House imesema kuwa rais wa Marekani Donald Trump amearifiwa kuhusu hali hiyo huko Annapolis. "Naziombea familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na wote waliopatwa na janga hilo," Donald trump ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana