Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Trump asaini sheria inayozuia watoto kutenganishwa na familia zao

media Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatano alisaini sheria inayoagiza familia za wahamiaji waliokamatwa kuwa kizuizini pamoja na watoto wasitenganishwi na wazazi wao. REUTERS/Leah Millis

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini sheria inayozuia watoto kutenganishwa na familia zao. Familia hizo ni wahamiaji ambao walivuka mpaka kinyume cha sheria na Mexico.

Utawala wa Marekani umekua ukikosolewa kutokana na hatua ya awali ya kutaka kutenganisha watoto hao na familia zao. Watoto zaidi ya 2,300 walitenganishwa na wazazi wao wiki tano zilizopita.

Rais Donald Trump na timu yake wamekua wakisema kwa siku kadhaa kuwa wanapaswa kutumia sheria ya kutenganisha watoto wa wahamiaji na familia zao. Hata hivyo baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho na Baraza la Wawakilishi, zoezi la kutenganisha watoto hao limesitishwa mara moja. Hatua hiyo ya awali ya Marekani ilikosolewa ulimwenguni kote hata nchini Marekani.

Rais wa Marekani alitangaza siku ya Jumatano wiki hii kuwa atasaini nakala hiyo ya kuzuia watoto kutenganishwa na familia zao, ambo ni wahamiaji waliovuka mpaka kinyume cha sheria kwenye mpaka na Mexico. "Ni muhimu sana kwangu [...] Tunataka familia kubaki pamoja. Ni muhimu sana, "alisema Donald Trump, akiisaini sheria hiyo katika ofisi yake, saa chache baada ya kutangaza kwamba atasitisha zoezi hilo ambalo limezua miguno na hasira ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na ndani ya chama chake.

Kwa upande wao, wabunge kutoka chama cha Democratic walikua walitangaza kwamba hawatopigia kura muswada huo wa sheria kuhusu wahamiaji ambao Rais wa Marekani anataka, kwa mujibu wa Anne Corpet, mwandishi wa RFI Washington, akinukuu maneno ya Joaqim Castro, mwakilishi wa chama cha Democratic katika jimbo la Texas: "Tunataka kutatua tatizo hili lakini hatutaki rais kutumia hoja yake mbaya kama kinga ili kupata idhni kutoka kwetu ya kujenga ukuta mpakani au kuwafukuza wahamiaji bila utaratibu wa kisheria. Ndio, tunakubali kutatua tatizo hili lakini hatuwezi kukubali kupitisha hoja zisizoeleweka za kujenga ukuta kwenye mpaka. "

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana