Pata taarifa kuu
GUATEMALA-VOLKANO-USALAMA

Idadi ya vifo kufuatia volkano yaongezeka na kufikia zaidi ya 73 Guatemala

Baada ya ugunduzi wa miili mingine miwili Jumanne wiki hii, idadi ya vifo kufuatia mlipuko wa Volkano ya Fuego (volkano ya Moto) nchini Guatemala imeongezeka na kufikia 75. Miili 23 ndio imetambuliwa hadi sasa.

Afisa wa polisi akitembea kwenye jivu lililosababishwa na mlipuko wa volkano Fuego, Guatemala.
Afisa wa polisi akitembea kwenye jivu lililosababishwa na mlipuko wa volkano Fuego, Guatemala. REUTERS/Luis Echeverria
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake Sergio Cabanas, mkurugenzi wa shughuli za dharura za uratibu wa kitaifa katika kupambana dhidi ya majanga (Conred) alisema siku ya Jumanne katika mkutano na waandishi wa habari kuwa "watu 192" ambao ana majina na maeneo wanakoishi , "walitoweka" tangu Jumapili Juni 3.

Mlipuko wa Volkano ya Fuego (Volkano ya moto), inayopatikana kilomita 35 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala, umesababisha maelfu ya watu kuhamishwa na uwanja wa ndege wa kimataifa umetakiwa kufungwa.

Mlipuko huo pia umewajeruhi watu 46 na kusababisha watu 3,271 kuyahama makaazi yao, kwa mujibu wa Conred. Aidha, watu 2,625 walilazimika kuhamishwa. Mlipuko wa vokano ya Fuego umeathiri jumla ya watu milioni 1.7 nchini Guatemala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.