Pata taarifa kuu
MEXICO-HAKI

Mexico: Kamati huru ya uchunguzi kuhusu kutoweka kwa wanafunzi kuundwa

Mahakama nchini Mexico imeagiza kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ili kujaribu kutoa mwanga juu ya kutoweka kwa wanafunzi 43 miaka minne iliyopita kusini mwa nchi hiyo. Mahakama imesema kuwa kuna mapungufu ya uchunguzi rasmi.

Kesi ya kutoweka kwa wanafunzi ni moja ya kashfa kubwa iliyoukumba utawala wa Enrique Peña Nieto.
Kesi ya kutoweka kwa wanafunzi ni moja ya kashfa kubwa iliyoukumba utawala wa Enrique Peña Nieto. REUTERS/Alejandro Acosta
Matangazo ya kibiashara

Mahakama imeitaka "Tume ya Ukweli na Haki" kukutana na wawakilishi wa waathirika, Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na ofisi ya mashtaka.

"Uchunguzi wa mwendesha mashitaka wa serikali haukua wa haraka wala wenye ufanisi, wala huru na bila ya upendeleo" kama inavyotakiwa na sheria ya kimataifa, imesema mahakama katika taarifa yake.

"Imeonekana kuwa kuna ushahidi mdogo unaopelekea kufikiria kwamba uamuzi na mashtaka dhidi ya watuhumiwa vilipatikana baada ya watuhumiwa kufanyiwa mateso," taarifa ya mahakama imeongeza.

Mnamo mwezi Machi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu alishtumu serikali ya Mexico kuhusika kuhusika katika vitendo vya mateso wakati wa uchunguzi.

Kulingana na toleo la serikali ya Mexico, maafisa wa polisi wanaojihusisha na rushwa waliwateka nyara wanafunzi 43 na kuwakabidhi kundi la wafanyabishara haramu ya madawa ya kulevya, ambalo lilipoteza miili yao kwa kuichoma moto kwenye mlima mkubwa wa taka taka wa Cocula, mji wa jimbo la Jalisco.

Kundi la wataalam wa kimataifa lilipinga madai hayo ya serikali katika ripoti iliyochapishwa mnamo mwaka 2015 na Mahakama ya Mexico pia inabaini kwamba "hakuna ukweli kwa madai hayo" na kwamba bado haijajulikana kwamba miili ya wanafunzi hao ilizikwa. Mahakama imeelezea masikitiko yake kuhusu "makosa mengi ya uchunguzi".

Kesi ya kutoweka kwa wanafunzi ni moja ya kashfa kubwa iliyoukumba utawala wa Enrique Peña Nieto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.