Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Korea Kaskazini yataka mazungumzo na Marekani kuendelea

media Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akikumbatiana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walipokutana katika eneo la mpaka la Panmunjom, 26 Mei 2018 The Presidential Blue House /Handout via REUTERS

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, anataka mkutano wake na rais wa Marekani Donald Trump kuendelea mwezi ujao nchini Singapore kama ilivyopangwa.

Kim Jong Un, amekutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, ambaye amesema uongozi wa Korea Kaskazini bado una nia ya kutokuwa na maeneo ya kutengeza silaha za nyuklia.

Kauli hii ya kiongozi huyo wa Kaskazini, imekuja wakati huu rais Trump akisema bado wanaendelea kuzungumza na maafisa wa Pyongyang na huenda mazungumzo hayo yakaendelea kama ilivyopagwa.

Wiki hii, rais Trump alijiondoa kwenye mazungumzo hayo, baada ya kusema kuwa, matamshi yenye ukali na yaliyoonekana kuwa ya  chuki, kutoka Korea Kaskazini yasingemwezesha kuja katika meza ya mazungumzo.

Hata hivyo, matamshi ya rais Trump siku ya Jumamosi kwamba mambo yanakwenda vizuri, huenda viongozi hao wakakutana tarehe 12 mwezi Juni kama ambavyo ilikuwa imepangwa.

Korea Kaskazini pamona na kutaka mkutano huo, imeonekana kutokubaliana na msimamo wa Marekani kuwa iachane  kabisa na mradi wake wa nyuklia, suala ambalo linaendelea kuwa tata.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana