Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Macron atoa mtazamo wake kwa bunge la Congress la Marekani

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelihotubia bunge la pamoja la Congress nchini Marekani na kukosoa sera ya rais Donald Trump ya Marekani kwanza.

Rais Macron akipigiwa makofi na Makamu rais Mike Pence na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan wakati akilihutubia baraza la Congress la Marekani Jumatano, Aprili 25, 2018.
Rais Macron akipigiwa makofi na Makamu rais Mike Pence na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan wakati akilihutubia baraza la Congress la Marekani Jumatano, Aprili 25, 2018. REUTERS/Aaron Bernstein
Matangazo ya kibiashara

Macron amesema sera hiyo, inatishia kutoendelea kwa dunia haraka.

Akipigiwa makofi na wabunge wa Marekani kwa muda wa dakika tatu, kiongozi huyo wa Ufaransa amesisitiza kuwa ni lazima Iran isiruhusiwe kuwa na silaha za nyuklia.

Makubaliano ya Marekani na Ufaransa kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mkataba mpya wa kuisitisha Iran kuendelea na mradi huo, umeikasirisha serikali ya Tehran.

Rais Hassan Rouhani amesema nchi yake haitashiriki kwa namna yoyote ile katika makubaliano mapya iwapo yatafanyika. Makubaliano ya sasa kati ya Tehran na Mataifa ya Magharibi kwa nchi hiyo kutoendelea na urutubishaji wa madini ya uranium kwa miaka 10 ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.