Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Amerika

Macron atoa mtazamo wake kwa bunge la Congress la Marekani

media Rais Macron akipigiwa makofi na Makamu rais Mike Pence na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan wakati akilihutubia baraza la Congress la Marekani Jumatano, Aprili 25, 2018. REUTERS/Aaron Bernstein

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelihotubia bunge la pamoja la Congress nchini Marekani na kukosoa sera ya rais Donald Trump ya Marekani kwanza.

Macron amesema sera hiyo, inatishia kutoendelea kwa dunia haraka.

Akipigiwa makofi na wabunge wa Marekani kwa muda wa dakika tatu, kiongozi huyo wa Ufaransa amesisitiza kuwa ni lazima Iran isiruhusiwe kuwa na silaha za nyuklia.

Makubaliano ya Marekani na Ufaransa kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mkataba mpya wa kuisitisha Iran kuendelea na mradi huo, umeikasirisha serikali ya Tehran.

Rais Hassan Rouhani amesema nchi yake haitashiriki kwa namna yoyote ile katika makubaliano mapya iwapo yatafanyika. Makubaliano ya sasa kati ya Tehran na Mataifa ya Magharibi kwa nchi hiyo kutoendelea na urutubishaji wa madini ya uranium kwa miaka 10 ijayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana